Simba Sports Club
News

Tupo tayari kuikabili JKT leo

8 Nov 2025

Tunashuka katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mechi zote mbili za Ligi Kuu tulizocheza tukishinda tena bila kuruhusu bao.

Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa JKT kutokana na aina ya kikosi walichonacho pamoja na benchi lao la ufundi lakini tumejipanga na tupo tayari kuwakabili.

Matola afunguka haya kuelekea mchezo huo.......

Kocha msaidizi, Seleman Matola amesema wachezaji wameandaliwa kimbinu na kisaikolojia kutokana na wapinzani tutakaokutana nao kwakuwa malengo yetu ni kushinda na kupata pointi tatu.

Matola ameongeza kuwa pamoja na upinzani ambao tunategemea kukutana nao lakini tupo tayari kuwakabili na tutaingia uwanjani kwa kutafuta mabao mengi huku tukijilinda vema tusiruhusu bao.

"Tunafahamu itakuwa mechi ngumu, tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa JKT, haijawahi kuwa mechi nyepesi kila tunapokutana lakini tupo tayari."

Advertisement

Wachezaji wapo tayari kwa mchezo

Mlinzi wa kati, Wilson Nangu amesema wachezaji wapo tayari kufuata maelekezo watakayopewa na walimu na kupambana muda wote wa mchezo ili kuisadia timu kupata alama tatu.

"Tunawaheshimu JKT lakini tupo tayari kuwakabili. Nitafurahi kucheza katika ardhi niliyoizoea lakini safari hii nitakuwa naisaidia timu yangu ya Simba kupata ushindi," amesema Nangu.

Hali ya kikosi....

Akizungumzia hali ya kikosi, Matola amesema mchezaji pekee ambaye hatakuwa sehemu ya mchezo kutokana na majeruhi ni mlinda mlango Moussa Camara huku wengine wote wakiwa tayari kuipambia timu.

Back to homepage
Share this story