Simba Sports Club
News

Tupo tayari kuikabili Fountain Gate

15 Apr 2026

Tutaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 3-1 tuliopata kwenye mchezo uliopita wa CRDB Federation Cup dhidi ya Dodoma Jiji Jumapili iliyopita.

Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu kwakuwa Fountain Gate ni timu imara inayoundwa na nyota wenye uzoefu ingawa hawapo katika nafasi nzuri kwenye msimamo.

Hatutaichukulia Poa Fountain Gate......

Kocha Mkuu, Steve Barker amesema pamoja na Fountain Gate kuwa katika mstari wa kushuka daraja kwenye Ligi Kuu lakini hatutaidharau kwa namna yoyote.

Barker amesema timu ambazo hazipo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo mara nyingi zikikutana na timu kubwa zinapambana kujikwamua kitu ambacho kinaongeza ugumu wa mchezo.

"Utakuwa mchezo mgumu na hatutaidharau hata kidogo Fountain Gate kwakuwa ipo chini kwenye msimamo bali tutaingia kwa tahadhari zote ili tupate alama tatu," amesema Barker.

Advertisement

Wachezaji wapo tayari......

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mshambuliaji, Seleman Mwalimu amesema maandalizi yamekamilika na wote wapo tayari kwa mchezo.

Mwalimu amesema kila mmoja anafahamu umuhimu wa kupata alama tatu kwenye mchezo huo ingawa tunafahamu utakuwa mgumu.

"Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa mchezo ambao tunafamu utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kupata alama tatu tatu," amesema Mwalimu.

Kapombe, Kagoma kuikosa Fountain Gate...

Nahodha wa timu, Shomari Kapombe na kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma hawatakuwa sehemu ya mchezo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano

Back to homepage
Share this story