Tutaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 tuliopata dhidi ya Tanzania Prisons Jumapili iliyopita.
Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Dodoma hasa kutokana na uimara wa kikosi chao.
Barker ataka soka safi na ushindi....
Kocha mkuu Steve Barker ameweka wazi kuwa anahitaji kuona kikosi chake kikitandaza soka safi lakini ushindi ndio lengo Kuu.
Barker ameongeza kuwa tunahitaji kuwa na muendelezo wa kupata alama tatu kwenye kila mchezo ili kujiweka katika nafasi nzuri za kupata ubingwa.
"Maandalizi yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri, tunajua tunaenda kukutana na timu ngumu lakini malengo yetu ni kuendelea kupata ushindi," amesema Barker.
Wachezaji wapo tayari kwa mchezo....
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia, David Kameta 'Duchu' amesema wapo tayari kufuata maelekezo watakayopewa na walimu ili kuhakikisha ushindi unapatikana kwenye mchezo wa leo.
"Kwa upande wetu wachezaji tumejiandaa vizuri na kila atakayepata nafasi kwenye atakuwa tayari kuipigania timu kupata matokeo chanya ugenini," amesema Duchu.