Simba Sports Club
News

Tupo Kamili kuivaa Prisons Leo

22 Feb 2026

Tutaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu chanya ya ushindi wa mabao 3-0 tuliopata katika mchezo wa hatua ya 64 bora ya michuano ya CRDB Federation Cup dhidi ya Green Land wiki iliyopita.

Mchezo wa leo ni muhimu kwetu kupata alama tatu ili kuendelea kuweka hai malengo yetu ya kuchukua ubingwa wa Ligi msimu huu.

Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Tanzania Prisons ambao wanaihitaji alama tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi lakini tumejipanga na tupo tayari kuwakabili.

Barker asisitiza soka safi na alama tatu.....

Kocha mkuu Steve Barker amesisitiza kuwa katika mchezo wa leo tunahitaji kuonyesha soka safi ili kuwafurahisha mashabiki na kupata alama tatu za kuendelea kupigania ubingwa.

Advertisement

"Maandalizi ya mchezo dhidi ya Prisons yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri, tunahitaji kushinda ili kuwapa furaha mashabiki na pia kupigania ubingwa wa Ligi," amesema Barker.

Wachezaji wapo tayari kwa mchezo....

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kati, Vedastus Masinde amesema wapo tayari kufuata maelekezo watakayopewa na walimu ili kuhakikisha ushindi unapatikana kwenye mchezo wa leo.

"Kwa upande wetu wachezaji tumejiandaa vizuri na kila atakayepata nafasi kwenye atakuwa tayari kuipigania timu kupata matokeo chanya ugenini," amesema Masinde.

Back to homepage
Share this story