Pamoja na ubora wa wapinzani huku tukifahamu tunacheza ugenini lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo chanya.
Tunafahamu haitakuwa mechi rahisi lakini malengo yetu ni kuimaliza leo ili kwenye mchezo wa marudiano nyumbani tusiwe na presha.
Meneja Pentev atoa msimamo....
Meneja Mkuu, Dimitar Pantev amesema kikosi kipo tayari kwa mchezo wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri ya kuiwakilisha Simba vema ugenini.
Pentev ameongeza kuwa pamoja na kupata takribani siku 20 ya kukinoa kikosi ameridhishwa na mapokeo ya wachezaji ya kile anachokifundisha kitu ambacho kinampa matumaini ya kufanya vizuri.
"Tunatarajia upinzani mkubwa kutoka kwa Nsingizini lakini timu ipo tayari kuhakikisha tunapata matokeo chanya ikiwezekana kuimailiza mechi ugenini," amesema Pentev.
Ahmed afunguka kuhusu hali ya hewa.....
Meneja Habari na Mawasiliano Ahmed Ally amesema kuna hali ya baridi kali hasa asubuhi na usiku lakini tayari wachezaji wameanza kuizoea.
Ahmed amesema faida tuliyonayo ni kwamba mechi itachezwa saa tisa Alasiri kwa saa za Eswatini sawa na saa 10 jioni nyumbani hivyo muda huo hakutakuwa na baridi.
"Ni kweli kuna baridi kali asubuhi na usiku lakini mechi inapigwa mchana kipindi ambacho kunakuwa kupo kawaida kwahiyo sioni changamoto yoyote ikitokea kwa wachezaji wetu na pia sio mara ya kwanza kukutana na hali ya hewa kama hii," amesema Ahmed.
Tumefika hatua hii baada ya kuitoa Gaborone United ya Botswana kwa jumla ya mabao 2-1 katika mechi mbili za nyumbani na ugenini.