Simba Sports Club
News

Tupo kamili kuikabili Namungo kwa Mkapa Leo

1 Oct 2025

Tutaingia kwenye mchezo huu tukiwa na kumbukumbu nzuri kufuatia ushindi wa mabao 3-0 tuliopata kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Fountain Gate.

Kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho jana na hakuna mchezaji aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa leo.

Kauli ya Kocha Matola.......

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Namungo kutokana na ubora walionao lakini hata hivyo tupo tayari kuhakikisha tunapata alama tatu.

Kuelekea mchezo huo Matola amesema kikosi kipo tayari isipokuwa tutaendelea kuwakosa Mohamed Bajaber na Abdulazak Hamza ambao bado ni majeruhi.

Advertisement

"Tupo tayari kuhakikisha tunapata alama zote tatu kwenye mchezo wa nyumbani, tunafahamu itakuwa mechi ngumu na mara zote tunapokutana na Namungo ushindani unakuwa mkubwa," amesema Matola.

Mligo afunguka kuhusu mchezo wa leo...

Mlinzi wa kushoto, Anthony Mligo amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na tupo tayari kuhakikisha ushindi unapatikana.

Mligo ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia Namungo amekiri kuwa utakuwa mchezo mgumu kwakuwa mara zote wanapocheza mechi kubwa wanakuwa na morali ya hali ya juu.

"Tunafahamu itakuwa mechi ngumu, Namungo ni timu imara lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo wetu wa nyumbani," amesema Mligo.

Back to homepage
Share this story