Simba Sports Club
News

Tupo Kamili 100% kuivaa Pamba Jiji

19 Mar 2026

Tutaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-1 tuliopata dhidi ya Singida Black Stars ugenini Machi, 11.

Tunafahamu haitakuwa mechi rahisi, tunakutana na timu ambayo inaundwa na nyota wengi bora lakini tupo tayari kupambana ili kupata alama tatu.

Barker afunguka kuhusu mchezo.....

Kocha Mkuu, Steve Barker amesema kikosi chetu kipo tayari kwa asilimia 100 kuelekea mchezo wa leo huku akiweka wazi utakuwa mgumu.

Barker ameongeza kuwa tumekuwa na ratiba ngumu hasa kutokana na kucheza mechi mfufulizo ugenini lakini hata hivyo tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi ili kuweza kufikia malengo tuliyojiwekea ya kupigania ubingwa.

Advertisement

"Tupo tayari kwa asilimia 100 kuwakabili Pamba Jiji, tunafahamu utakuwa mchezo mgumu hasa kutokana na wapinzani kuwa na matokeo mazuri wakiwa nyumbani lakini tumejiandaa kimwili na kiakili ili kuweza kuwakabili," amesema Kocha Barker.

Morice nae atia neno .....

Kiungo mshambuliaji, Morice Abraham amesema pamoja na upinzani na ugumu ambao tunatarajia kukutana nao lakini tumejipanga na malengo yetu yanabaki yale yale ya kutafuta alama tatu.

"Tunawaheshimu Pamba na tunategemea watatupa upinzani mkubwa lakini tupo hapa na lengo ni moja tu kupata alama tatu," amesema Morice.

Back to homepage
Share this story