Tutaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 2-1 tuliopata dhidi ya Coastal Union siku ya Jumamosi.
Tunaamini utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa Singida lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.
Hiki ndicho alichosema Kocha Matola......
Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri morali ipo juu na kila mchezaji anajua umuhimu wa ushindi kwenye mchezo wa leo.
Matola amesema tunawaheshimu Singida kutokana na ubora walionao na tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.
"Timu iko tayari kwa mchezo wa kesho, wachezaji wapo kwenye hali nzuri na maandalizi yanaendelea.
Mechi zetu za nyumbani zimehamishiwa Chamazi.....
Kwa sasa mechi zetu za nyumbani zitapigwa Uwanja wa Azam Complex kutokana na ule wa Jamhuri mkoani Morogoro kuwanyima wenye haki ya kurusha vizuri matangazo Mubashara (Azam TV) sababu ya miundombinu yake kutokuwa rafiki.
Tuliwafunga 2-1 Uwanja wa Liti
Katika michezo wa mzunguko wa uliofanyika Uwanja wa Liti Oktoba 8, tuliwafunga mabao 2-1.
Mabao yetu yalifungwa na na Saido Ntibazonkiza na Moses Phiri huku lile la Singida likifungwa na Deus Kaseke.