Mtendaji mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa kesho tunahitaji jambo moja tu ambalo ni kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ili kuweka heshima kwa Taifa.
Barbara amesema hakuna kitu kingine tunahitaji zaidi ya kufuzu makundi ili kuleta furaha kwa nchi na Wanasimba ambao wana matarajio makubwa nasi.
Barbara amesema kikosi kimechukua tahadhari zote za Covid-19 ili kuepusha njama ambazo zinaweza kufanywa na wapinzani ingawa hakuna dalili za kufanyika.
"Tulivyotaka nyumbani wote tulipimwa tukakutwa tupo sawa na huku tumepimwa majibu yatatoka baadae na tunaamini yatabaki hivyo na mwalimu kesho atakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi chake," amesema Barbara.
Barbara amesema hali ya hewa ya Zambia ni sawa na Dar es Salaam hivyo hakuna atahari zozote za kimazingira ambazo watakutana nazo wachezaji wetu.