Simba Sports Club
News

Tunaanza 'Kutesti Mitambo' Jumatatu

21 Jul 2024

Mchezo huo utakuwa wa kwanza wa kocha Fadlu Davids kukiongoza kikosi chetu na kitampa mwanga ni jinsi gani wachezaji wake wameshika vizuri mazoezi anayowapa.

Sehemu kubwa ya kikosi chetu kinaundwa na wachezaji wengi wageni hivyo itampa nafasi kocha Fadlu kuona jinsi gani wanazoeana vizuri na wenzao.

Advertisement

Mechi nyingine ya kirafiki ambayo imethibitishwa itakuwa Julai 29, dhidi ya Al-Adalah FC inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Saudi Arabia.

Kutoka mechi ya El- Qanah hadi Al-Adalah kuna takribani wiki moja hivyo tunaangalia uwezekano wa kupata michezo mingine ya kirafiki kabla ya timu kurejea nyumbani.

Back to homepage
Share this story