Shomari Kapombe alitupatia bao la kwanza dakika ya nne baada ya shuti kali lililopigwa na Steve Mukwala kugonga mwamba kabla ya kumkuta mfungaji.
Kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu alishindwa kuendelea na mchezo na kufanyiwa mabadiliko dakika ya 31 baada ya kupata maumivu nafasi yake ikachukuliwa na Jean Charles Ahoua.
Ahoua alitupatia bao la pili dakika ya 33 kwa shuti kali la chini chini akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mukwala.
Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kuzidi kuliandama lango la Namungo lakini safu yao ya ulinzi ilikuwa imara.
Debora Fernandes alitupatia bao la tatu dakika ya 86 kwa shuti kali la mguu wa kushoto baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Leonel Ateba.
Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 19 tukiwa nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kucheza mechi nane.
X1: Camara, Kapombe, Nouma (Zimbwe Jr' 67'), Chamou, Che Malone, Ngoma (Mzamiru 67'), Mutale (Fernandez 56'), Okajepha, Mukwala, Awesu (Ahoua 31'), Chasambi
Walioonyeshwa kadi: Nyenye 59'
X1: Nahimana, Kibailo, Mlingo, Amade, Nyoni, Nyenye, Masawe, Domayo (Hamza 78'), Jofrey (Kagere 45') Buswita, Kabunda