Simba Sports Club
News

Tumezindua jezi zetu za msimu 2023/24 juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro

21 Jul 2023

Kama kawaida tumezindua jezi za aina tatu Nyekundu kwa mechi za nyumbani, Nyeupe ugenini na bluu kama jezi namba tatu.

Mara tu baada ya uzinduzi huu jezi zinapatikana kwenye maduka yote ya mzabuni wetu Sandland The Only One nchi nzima.

Tumeweka utaratibu mzuri wa upatikanaji wa jezi ambapo zitauzwa jumla kupitia kwenye matawi yetu na watu binafsi ambapo inatakiwa kununua pisi 108.

Advertisement

Bei ya jumla ni Sh. 32,000 ambapo utanunua kuanzia pisi 108 wakati rejareja itakuwa Sh. 40,000.

Tumeweka utaratibu huu ili kurahisisha upatikanaji wa jezi na kuwapa nafasi Wanasimba kupata jezi mapema bila usumbufu.

Back to homepage
Share this story