Simba Sports Club
News

Tumewapa furaha tuliyowaahidi Wanasimba

8 Aug 2022

Kibu Denis alitupatia bao la kwanza dakika ya 19 kwa shuti kali ndani ya 18 lililomshinda mlinda mlango wa St. George baada ya shambulizi lililoanzia katikati ya uwanja.

Baada ya bao hilo St.George waliongeza mashambulizi langoni kwetu ambapo dakika ya 23 almanusura wasawazishe lakini mpira wa kichwa uliopigwa na kiungo wao ulitoka nje kidogo ya lango.

Nelson Okwa alitupatia bao la pili dakika ya 59 muda mfupi baada ya kuingia kutokea benchi akimalizia pasi ya Clatous Chama ambaye alimpiga chenga mlinzi wa St.George.

Advertisement

Baada ya bao hilo tuliendelea kuliandama lango la St.George huku tukitawala sehemu kubwa na kuwafanya mashabiki kulipuka kwa shangwe.

Kocha Zoran Maki aliwaingiza Clatous Chama, Vincent Akpan, Nelson Okwa, Peter Banda, Dejan Georgijevic, Mzamiru Yassin,Moses Phiri Shomari Kapombe na kuwatoa Kibu, Sadio Kanoute, Augustine Okrah, Jonas Mkude, Habib Kyombo, Israel Patrick, Mohamed Hussein na Pape Sakho.

Back to homepage
Share this story