Simba Sports Club
News

Tumetoka sare na Bunda Queens

22 Jan 2024

Mchezo huo ulikuwa mkali huku tukimiliki sehemu kubwa na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini hatukuweza kuzitumia.

Wenyeji Bunda walikuwa wakifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini hata hivyo tulikuwa makini kuhakikisha tunawadhibiti.

Advertisement

Kocha Msaidizi Mussa Hassan Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Danai Bhobho, Jentrix Shikangwa na Asha Djafar na kuwaingiza Dotto Evarist, Ritticia Nabbosa na Mwanahamisi Omary.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha pointi 13 tukiendelea kusalia nafasi ya pili.

Back to homepage
Share this story