Tulianza kwa kasi mchezo huo huku tukifika zaidi langoni mwa Fassell katika dakika 20 za mwanzo lakini ufanisi wa nafasi tulizotengeneza hakuwa wa asilimia 100.
Kiungo mshambuliaji Joshua Mutale alikuwa mwiba mkali kwa safu ya ulinzi ya Fassel huku akitengeneza nafasi kadhaa ambazo hazikutumika vizuri.
Jonathan Sowah alitupatia bao hilo pekee dakika ya 27 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Steven Mukwala aliyekuwa nje ya 18 na kuwazidi ujanja walinzi Fassell na kuingia mpira ndani ya boksi kabla ya kutoa pasi kwa mfungaji.
Dakika ya 34 Fassell walisawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi Hussein Mbegu kufanya madhambi ndani ya 18.
Dakika ya 68 kocha Fadlu Davids alifanya mabadiliko ya kuwatoa Awesu Awesu na Bashiru Salum na kuwaingiza Naby Camara na Morice Abraham.
Baada ya mabadiliko hayo tuliendelea kufanya kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Fassell lakini hata hivyo hatukuweza kupata bao la pili.
Dakika ya 80 tulifanya mabadiliko mengine ya kuwatoa Mukwala na Sowah na kuwaingiza Valentino Mashaka na Kibu Denis.
Mchezo huo ni wa mwisho wa kirafiki tukiwa Misri kabla ya kikosi kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam kesho.