Simba Sports Club
News

Tumetoa msaada Kituo cha CHAKUWAMA

30 Jan 2026

Huu ni utaratibu tuliyojiwekea wa kurejesha kwa jamii ikiwa ni kuomba baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu atufungulie kila tunapoelekea kucheza mechi za Kimataifa kama Jumapili dhidi ya ES Tunis.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema pamoja na uwezo wa wachezaji na benchi la ufundi lakini bila msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu hatuwezi kufika mbali ndio maana tumekuwa na utaratibu wa kutoa misaada kwa wenye uhitaji.

"Leo tupo hapa kwa ajili ya kutoa misaada kwa Kituo hiki cha CHAKUWAMA lengo ni kumuomba Mwenyezi Mungu atujalie tufanye vizuri. Sote tunafahamu tutakuwa na mchezo mgumu siku ya Jumapili ndio maana tunaomba msaada kutoka kwa Mungu," amesema Ahmed.

Kwa upande wake mlezi mkuu wa Kituo hicho, Hassan Hamis ameishukuru Simba kwa msaada huo huku akituombea kwa Mungu atuwezeshe kupata matokeo ya ushindi siku ya Jumapili.

Advertisement

Nae mwakilishi kutoka Mo Dewji Foundation, Neema Kizigha amesema wataendelea kushirikiana na Uongozi wa klabu kutoa misaada kwa wenye uhitaji kwakuwa ni baraka kwa Mungu kuwakumbuka wenye uhitaji.

"Mo Dewji Foundation tutaendelea kuwa pamoja na Uongozi wa klabu ili kuzidi kuvifikia vituo vingi kwa ajili ya kuwapa tabasamu watoto wetu," amesema Bi. Neema.

Akizungumza kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Mjumbe wa Bodi, Seleman Haroub amesema Simba kila jambo tunalofanya lazima tumshirikishe Mungu na hii haitaishia hapa kikubwa tunahitaji kupata matokeo ya ushindi.

Back to homepage
Share this story