Khelffin Salim aliipatia Dodoma bao la kwanza dakika ya tisa kwa mguu wa kushoto akiwa nje ya 18 baada ya walinzi wetu kuchelewa kuondoa mpira wa hatari.
Baada ya bao hilo tulifanya mashambulizi mengi langoni mwa Dodoma lakini ufanisi wetu kwenye kuzitumia nafasi tulizo tengeneza haukuwa kwa asilimia 100.
Seleman Mwalimu alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 54 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi kutoka kwa Nickson Kibabage akiwa ndani ya kisanduku cha sita.
Anicet Oura alitupatia bao la pili dakika ya 59 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Clatous Chama.
Mwalimu alitupatia bao la tatu dakika ya 67 kwa shuti kali la mguu wa kushoto baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Dodoma kufuatia kupokea pasi ya Neo Maema.
X1: Kassali, Kapombe, Kibabage (Mligo 81'), Toure (Mbegu 75') De Reuck, Kagoma, Gueye, Maema (Loemba 70'), Mwalimu (Mpanzu 75'), Chama, Oura (Chasambi 81')
Waliionyeshwa kadi: Libasse 66' Kagoma 80' Kapombe 82'
X1: Mgore, Augustino, Bikoko, Hoza, Anderson, Mwana, Kipagwile (Mgaza 58'), Munganga, Khelffin (Milandu 68'), Gadiel, Kayanda (Edgar 51')
Waliionyeshwa kadi: Hoza 33' Khelffin 55'