Fufuni walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Mboni Steven dakika ya 14 kwa shuti kali nje 18 baada ya kupokea pasi kutoka upande wa kulia.
Hussein Mbegu alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 22 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Joshua Mutale.
Kocha mkuu Steve Barker alifanya mabadiliko ya kuwaingiza nyota wanne Neo Maema, Daud Semfuko, Naby Camara, Benjamin William wakichukua nafasi za Joshua Mutale, Allasane Kante, Mzamiru Yassin na Awesu Awesu.
Dakika ya 74 Barker alifanya mabadiliko ya kumtoa Amiri Yondani na kumuingiza Anthony Mligo ili kuongeza ufanisi upande wa kushoto.
Naby Camara alitupatia bao la pili kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa nje ya 18 dakika ya 90 baada ya krosi iliyopigwa na Elie Mpanzu kuzuiliwa na walinzi wa Fufuni.
Mchezo wetu nusu fainali utakuwa dhidi ya Azam FC utakaopigwa Alhamisi Januari, 8 katika Uwanja wa New Amaan Zanzibar.