Tumepata nafasi hiyo kwa jumla ya mabao 3-0 kutokana na ushindi tuliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Jumapili iliyopita nchini Eswatini.
Nsingizini walianza mchezo kwa kasi ambapo dakika 10 za mwanzo walifika zaidi langoni kwetu huku mlinda mlango Yakoub Suleiman akifanya kazi kubwa ya kuokoa michomo.
Kuanzia dakika ya 15 tuliuchukua mchezo huku tulifanya mashambulizi mengi langoni mwa Nsingizini ingawa ufanisi wa kuzitumia ilikuwa mdogo.
Kipindi cha pili tulirejea kwa kasi huku Meneja Mkuu Dimitar Pantev akifanya mabadiliko ya wachezaji watano lakini hata hivyo hatukuweza kupata bao.
X1: Yakoub, Duchu, Mligo, Chamou, De Reuck, Kagoma(Kante 57'), Mutale (Awesu 87') (Mukwala 57'), Morice, Kibu, Ahoua (Maema 57') Mpanzu (Sowah 57')
Waliionyeshwa kadi: Duchu 65' Kibu 70'
X1: Thabo, Dlamini, Ade, Madondo (Msuvelelo 71') Mavuso, Thwala, Khumalo (Vermark 71') Kwakye, Macina (Gadlela 55') Shongwe, Dlamini
Waliionyeshwa kadi: