Tulianza mchezo taratibu huku wapinzani Gaborone wakifika zaidi langoni kwetu ingawa tulikuwa imara kudhibiti mashambulizi yao.
Jean Charles Ahoua alitupatia bao la kwanza dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati baada ya Morice Abraham kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Lebakhan Ditsele aliisawaziahia Gaborone United kwa mkwaju wa penati dakika ya 58 baada ya Karaboue Chamou kumfanyia madhambi Maponda.
Tumetinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia ushindi wa bao moja tuliopata ugenini wiki iliyopita.
X1: Camara (Yakoub 77'), Kapombe, Mligo, Chamou, De Reuck, Kagoma, Morice, Kante, Sowah (Mukwala 55') Ahoua (Mutale 72'), Mpanzu (Kibu 78')
Waliionyeshwa kadi: Sowah 51' Chamou 56' Camara 71'
X1: Motswagole, Velaphi, Ivan, Gora, Johnson, Ditsele, Phiri ,Kgwasane, Sesay (Maponda 45') Ramoagi (Chideu 78'), Kgamanyane
Waliionyeshwa kadi: Ivan 81' Kgamanyane 87'