Tulianza mchezo kwa kasi tukiliandama lango la Green land huku tukitengeneza nafasi zaidi ya tano katika dakika 10 za mwanzo.
Baraka Mwangosi alitupatia bao la kwanza dakika ya 12 baada shuti kali lililopigwa na Neo Maema kupanguliwa na mlinda mlango wa Green land kabla ya kumkuta mfungaji.
Mlinzi wa kushoto Anthony Mligo alitupatia bao la pili dakika ya 48 kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi kutoka kwa Maema.
Kipindi cha pili tulirejea kwa kasi huku tukifika mara nyingi langoni mwa Green land lakini mashambulizi yetu yaliishia katika safu ya ulinzi.
Neo Maema alitupatia bao la tatu dakika ya 89 baada ya mpira wa krosi uliopigwa na David Kameta 'Duchu' kuokolewa kwa kichwa na mlinzi wa Green Land kabla ya kumkuta mfungaji.
X1: Abel, Kapombe (Duchu 62') Mligo, Mbegu, Masinde, Semfuko (Naby 87'), Gueye (Chasambi 79'), Maema, Mwangosi.(Mwalimu 79'), Loemba, Mpanzu (Bashiru 62')
Waliionyeshwa kadi: