Simba Sports Club
News

Tumetinga 16 bora ya CRDB Federation Cup

7 Mar 2026

Tulianza mchezo huo kwa kasi huku tukiliandama lango la B19 na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini tulikosa umakini wa kuzitumia.

Inno Loemba alitupatia bao la kwanza kwa kichwa baada mpira wa krosi uliopigwa na Libasse Gueye kumponyoka mlinda mlango wa B19 kabla ya kumkuta mfungaji.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi huku tukitengeza nafasi na kufanya mashambulizi mengi lakini bado hatukuzitumia vizuri.

Clatous Chama alitupatia bao la pili dakika ya 76 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya Elie Mpanzu.

Advertisement

Ushindi huu unatufanya kukutana na Dodoma Jiji katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano hii.

X1: Abel, Duchu, Mligo, Toure, Masinde, Naby (Semfuko 58') Gueye (Oura 58'), Kante, Loemba (Mwangosi 78'), Morice (Chama 70'), Kibaila (Mpanzu 58')

Waliionyeshwa kadi: Gueye 34'

Back to homepage
Share this story