Simba Sports Club
News

Tumeshusha kocha wa makipa kutoka Morocco

4 Aug 2022

Kabla ya kujiunga na kikosi chetu Mohamed alikuwa Kocha wa Timu ya Vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Al Ain Sports Club ya Falme za Kiarabu (UAE) huku pia akisimamia baadhi ya mechi za timu ya wakubwa.

Kocha Mohamed amefundisha timu za madaraja mbalimbali Falme za Kiarabu kwa miaka 18 tangu alipokwendwa mwaka 2004 akitokea Timu ya F.S.B inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Morocco akiwa kocha msaidizi.

Advertisement

Kocha Mohamed anajua kuongea kwa ufasaha lugha za Kiarabu, Kiingereza na Kifaransa.

Mohamed anachukua nafasi ya Tyron Damons ambaye ameondoka klabuni baada ya kumalizika msimu uliopita.

Back to homepage
Share this story