Uongozi wa Simba umejiridhisha juu ya ubora na uzoefu wa Kocha Zoran hasa katika soka la Afrika ambacho ndicho kigezo kikuu kilichozingatiwa katika kumuajiri.
Kabla ya kuja kwetu Zoran (60) alikuwa anaifundisha Al Tai FC ya Saudi Arabia ambayo alijiunga nayo aikitokea CR Belouizdad ya Algeria na kuiwezesha kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Zoran pia amewahi kuinoa Wydad Athletic Club ambayo ni miamba ya soka nchini Morocco.
Mwaka 2018 aliifikisha Primeiro De Agosto ya Angola Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.
Kocha Zoran si mgeni kwa Tanzania amewahi kuja na Timu ya Al Hilal ya Sudan na kushiriki mashindano ya Super Cup yaliyoandaliwa na Simba mwaka jana.
Malengo tuliyompa Kocha Zoran ni kuhakikisha anatufikisha Nusu Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na kuurejesha ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la Azam Sports.
Kocha Zoran anatarajiwa kuanza kazi mapema kwenye maandalizi ya msimu (Pre Season) ambayo tutaitangaza hivi karibuni.