Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku Azam wakifanya mashambulizi makali zaidi katika dakika 10 za mwanzo.
Katika kipindi cha robo ya pili ya mchezo nyota wetu walitulia na kuonekana kupanga mashambulizi lakini kikwazo kikawa kuipenya safu ya ulinzi ya Azam.
Mlinzi wa kati, Lameck Lawi aliipatia Azam bao hilo pekee dakika ya 73 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Chekhina Diakite.
Mlinzi wa kulia David Kameta 'Duchu' alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya tatu ya nyongeza kipindi cha pili.
X1: Abel, Duchu, Mligo, Chamou, De Reuck, Kante (Semfuko 69), Ahoua, Naby, Sowah (Mwangosi 45') Maema (Bajaber 45') Mpanzu (Mukwala 77')
Waliionyeshwa kadi: Chamou 22' Duchu 59' 90+3 (Nyekundu) Naby 63'
X1: Manula, Chilambo, Zouzou, Lawi, Twalib, Himid, Zidane (Bakwayima 63'), Kibeku (Byiobia 37') Kitambala, Akaminko, Diakite
Waliionyeshwa kadi: Sereri 6' Zouzou 45+4' Lawi 46' Akaminko 57' Himid 78'