Simba Sports Club
News

Tumeshinda mechi ya kirafiki dhidi ya Wadi Degla

26 Aug 2025

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishamnuliana kwa zamu lakini tulimiliki sehemu kubwa karibia kila eneo.

Licha ya mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa timu zote lakini hakuna timu iliyopata bao katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko ya wachezaji wawili ambapo walitoka

Morice Abraham na Steven Mukwala na kuingia Bashiru Salum na Jonathan Sowah ambao kwa kiasi kikubwa waliongeza kasi kubwa.

Advertisement

Elie Mpanzu alitupatia bao la kwanza dakika ya 73 baada ya kukokota mpira kutoka katikati ya uwanja na kutandika shuti kali lililomshinda kipa wa Wadi aliyebaki anashangaa mpira huo uliotinga moja kwa moja nyavuni.

Dakika 74 kocha Fadlu Davids alifanya mabadiliko mengine ya kuwatoa Naby Camara, Mpanzu na Neo Maema na kuwaingiza Abraham, Anthony Mligo na Joshua Mutale ‘Budo’

Kibu Denis alitupatia bao la pili dakika ya 79 akiwa ndani ya boksi akaunganisha kwa mtindo wa tikitaka kwa kutumia mguu wa kushoto na mpira wa krosi uliopigwa na Jean Charles Ahoua.

Kesho kikosi chetu kitacheza mechi ya mwisho ya kirafiki dhidi ya FC Fassel ambayo ni Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Liberia.

Back to homepage
Share this story