Simba Sports Club
News

Tumerejea Nyumbani kuikabiribisha TRA United uxs

22 Mar 2026

Kabla ya mchezo wa leo tumetoka kucheza dhidi ya Pamba Jiji, Singida Black Stars, Yanga, Dodoma Jiji na Tanzania Prisons zote zikiwa ugenini.

Mashabiki wetu wa jijini Dar es Salaam baada ya kipindi cha takribani mwezi mzima kuiona timu yao kupitia luninga leo watapata nafasi ya kuitazama Mubashara kutoka Meja Jenerali Isamuhyo.

Kocha Barker afunguka mengi kuelekea mchezo.......

Kocha mkuu, Steve Barker amesema amewafuatilia TRA katika mchezo wao uliopita dhidi ya watani na kujiridhisha kuwa ni timu imara na tunatarajia kupata upinzani mkubwa.

Kuhusu maandalizi kocha, Barker amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri jana wamefanya mazoezi mwisho na hakuna ambaye amepata changamoto ambayo itamfanya kuukosa mchezo.

"Maandalizi ya mchezo yamekamilika, wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri. Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunawaheshimu TRA lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi nyumbani," amesema Kocha Barker.

Advertisement

Kibabage afunguka kwa niaba ya wachezaji......

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kushoto, Nickson Kibabage amesema pamoja na ugumu ambao tunategemea kukutana nao lakini tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunapata kupata ushindi nyumbani.

"Kwa upande wetu kama wachezaji kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anapambana mpaka mwisho kuisaidia timu kupata ushindi," amesema Kibabage.

Tunaanza Mzunguko wa pili wa Ligi Leo....

Mchezo wetu wa leo utakuwa ni wa 14 wa Ligi Kuu ya NBC lakini utakuwa ni wa kwanza wa mzunguko wa pili huku tukiwa na michezo miwili mkononi.

Back to homepage
Share this story