Simba Sports Club
News

Tumepoteza ugenini dhidi ya ES Tunis

24 Jan 2026

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini mashambulizi mengi yaliishia kwenye idara ya ulinzi.

Jack Diarra aliipatia ES Tunis bao hilo pekee dakika ya 21 baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa nahodha Hmida na kumzidi ujanja Shomari Kapombe.

Baada ya bao hilo kikosi chetu kiliongeza umakini na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini ufanisi wa kuzitumia haukuwa mkubwa.

Januari 30 tutacheza mechi ya marudiano dhidi ya ES Tunis katika mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Advertisement

X1: Ben Said, Keita IB, Laifin. N, Ben Hmida, Jelassi.H, Onuche.O, Konate.A (Booulia 63') TKA.H, Yan Sasse (Rafia 88'), Diarra.J (Jebali 77'), Diakite.A (Danho 63')

Waliionyeshwa kadi:

X1: Kassali, Kapombe, Kibabage (Masinde 81'), Nangu, De Reuck, Kagoma, Kibu (Mwalimu 70'), Naby (Maema 81'), Sowah (Gueye 45'), Morice (Chama 45') Mpanzu

Waliionyeshwa kadi: Nangu 55' Gueye 90+2'

Back to homepage
Share this story