Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini umakini kwenye kutumia nafasi zilizopatikana ikiwa changamoto.
Kiungo mshambuliaji, Morice Abraham alimanusura atupatie bao dakika ya 22 baada ya mpira wake kutoka nje ya lango kufuatia kazi nzuri iloyofanywa na Joshua Mutale.
Bernado Oliveira aliipatia Petro De Luanda bao la kwanza dakika ya 77 baada kupiga shuti la chini chini nje ya 18 lililomgonga Rushine De Reuck na kumchanganya mlinda mlango Yakoub Suleiman.
Baada ya bao hilo tuliongeza kasi ya kutaka kusawazisha lakini Petro ambao muda mwingi walikuwa nyuma walikuwa makini kuondoka hatari.
Mchezo wetu wa pili wa hatua ya makundi utakuwa Jumapili Novemba 30 ugenini dhidi ya Stade Malien ya Mali.
X1: Yakoub, Kapombe, Mligo, Nangu, De Reuck, Kante (Mukwala 83') Morice (Chasambi 73') Naby (Ahoua 52') Mutale (Sowah 52') Maema, Mpanzu
Waliionyeshwa kadi: Ahoua 89'
X1: Hugo, Anderson, Ruben, Toro, Benny (Maya 87'), Jo Paciencia (Reis 63') Pareira, Kinito, Eddie, Hossi (Vidinho 85') Gigal (Gilberto 63')
Waliionyeshwa kadi: Kinito 20' Toro 60'