Simba Sports Club
News

Tumepoteza Ngao ya Jamii mbele ya JKT

12 Oct 2025

Wilfred Gerrard aliipatia JKT bao la kwanza dakika ya 12 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Simba Queens.

JKT walipata bao la pili dakika ya 16 baada ya mlinzi Asha Omary kujifunga wakati akiokoa mpira wa krosi uliopigwa na Sarah Joel.

Mabao hayo yalidumu kwa dakika zote 45 za kipindi cha kwanza ambapo licha ya kosa kosa lakini hakuna kilichobadilika.

Advertisement

Kipindi cha pili Queens walirudi kwa kasi kusajaribu kutafuta mabao ya kusawazisha lakini JKT walikuwa makini kuhakikisha nyavu zao haziguswi.

Zawadi Usanase alitupatia bao dakika ya mwisho ya mchezo baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Jentrix Shikangwa.

X1: Ruth Aturo, Zainah Nandede, Dotto Evarist (Adhiambo 84') Esther Mayala, Ruth Ingosi, Zanga Brice, Elizabeth Wambui, Vivian Corazone (Zawadi 66') Cynthia Shilwatso (Amarachi 66'), Asha Omary (Jentrix 40'), Aisha Mnunka

Back to homepage
Share this story