Stade Malien walipata bao la kwanza dakika ya 15 kupitia kwa Thaddeus Nkeng baada ya kumalizia pasi ya kichwa iliyopigwa Ousmane Coulibaly akiwa ndani ya sita.
Ismail Simpara aliipatia Stade Malien bao la pili dakika ya 23 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona na Diallo.
Kipindi cha pili tulirejea kwa kasi ambapo dakika ya 50 Jonathan Sowah alipoteza nafasi ya wazi baada ya kushindwa kumalizia mpira uliopigwa na Neo Maema.
Neo Maema alitupatia bao la kwanza kwa shuti kali nje ya 18 dakika ya 54 baada ya kumalizia mpira wa Shomari Kapombe.
Mlinda mlango Yakoub Suleiman alicheza mkwaju wa penati uliopigwa na Nkeng dakika ya 61 baada ya yeye mwenyewe kufanya madhambi ndani ya 18.
Kiungo wa kati, Allasane Kante alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 82 baada ya kumchezea madhambi Simpare ambaye alikuwa akielekea kufunga.
Matokeo haya yanatufanya kupoteza mechi zote mbili za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya wikiendi iliyopita kufungwa moja nyumbani dhidi ya Petro De Luanda.
X1: Traore, Awine, Simpara, Diarra, Dobe, Bello, Camara (Haman 57') Traore (Bagayoko 75') Coulibaly, Diallo (Konare 74') Nkeng (Simpara 78')
Waliionyeshwa kadi:
X1: Yakoub, Kapombe, Mligo, Nangu, De Reuck (Chamou 45'), Naby, Mutale (Kante 45') Maema, Mwalimu (Sowah 45') Ahoua (Morice 45') Mpanzu
Waliionyeshwa kadi: Sowah 45' Yakoub 59' Kante 82' nyekundu, Camara 90'