Simba Sports Club
News

Tumepoteza mbele ya wenyeji ASFAR

30 Oct 2022

Mchezo ulianza kwa kasi ya kadiri huku timu zikishambuliana kwa zamu huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja

Ibtissam Jraidi aliwapatia wenyeji bao la kwanza dakika 66 kwa kichwa akimalizia mpira mrefu wa krosi uliopigwa na mlinzi wa kushoto Ghizlane Chebbak.

Advertisement

Baada ya bao hilo tulitengeza nafasi na kufanya mashambulizi kadhaa lakini tulikosa umakini wa kumalizia.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Koku Kipanga na Olaiya Barakat kuchukua nafasi za Vivian Corazone na Pambani Kuzoya.

Back to homepage
Share this story