Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini walikosa umakini wakutumia nafasi walizopata.
Pamoja na mashambulizi hayo ya pande zote timu hizo zilienda mapumziko bila ya yoyote kupata bao.
Advertisement
Ihefu walipata bao hilo la ushindi kupitia kwa Beny Ng'wavi dakika ya 67 kwa kichwa akimalizia mpira krosi kutoka upande wa kulia.
Kikosi chetu kitacheza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi keshokutwa Jumatatu dhidi ya Azam FC.