Al Hilal walianza mchezo kwa kasi ambapo ndani ya dakika 10 za mwanzo walipata mabao mawili kupitia kwa Adama Coulibaly na El Hadji Madike baada ya kutumia vizuri nafasi walizopata.
Elie Mpanzu alitupatia bao la kwanza dakika ya 24 kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango wa Al Hilal, Farid.
Kipindi cha pili Al Hilal walirejea wakiwa watulivu na makini kwa mashambulizi tuliyokuwa tunafanya huku wakija kwetu mara chache lakini kwa nguvu kubwa.
Al Hilal walipata bao la tatu ya 54 kupitia kwa Sunday baada ya kiungo mkabaji, Allasane Kante kupokonywa mpira uliopelekea kuruhusu kufungwa.
Dakika ya 70' Al Hilal walipata bao la nne kupitia Sunday tena alilofunga kwa kuwatoka walinzi na kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango Alexander Erasto.
X1: Abel (Alexander 45'), Kapombe (Duchu 45') Mligo, Nangu (Vedastus 45'), Rushine (Chamou 45'), Camara(Kante 45' Semfuko 80'), Maema (Awesu 45'), Ahoua (Kibu 45'), Mwalimu (Sowah 45') Mutale (Mzamiru 45'), Mpanzu (Kibaila 45' Chasambi 80')
X1: Farid, Fares, Simbo, Diof, Ebuela, Luzolo, Madike, Fofana, Coulibaly, Cole, Sunday