Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu ingawa tulimiliki zaidi mpira na kufika mara nyingi langoni mwa Azam lakini ufanisi wa kutumia nafasi tulizopata ulikuwa mdogo.
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Azam lakini bado tulishindwa kutumia nafasi tulizopata
Japhet Kitambala aliwapatia Azam bao la kwanza dakika ya 83 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Nasoro Saadun.
Idd Nado aliwapatia Azam bao la pili dakika ya 88 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Saadun tena.
Baada ya mchezo huu Ligi Kuu ya NBC itasimama kwa mwezi mmoja kupisha michuano ya AFCON.
X1: Yakoub, Kapombe, Mligo, Nangu, Chamou, Kagoma, Mutale (Kibu 63') Kante (Sowah 84'), Mukwala (Mwalimu 63'), Morice, Mpanzu
Waliionyeshwa kadi: Kante 42'
X1: Foba, Mwaikenda, Msindo, Yoro, Zouzou, Kanoute (Akaminko 67'), Sereri (Saadun 67') Himid, Kitambala, Feisal, Nado
Waliionyeshwa kadi: Diaby 33' Himid 73'