Simba Sports Club
News

Tumepoteza...

26 Jan 2022

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja.

Tulianza mchezo kwa kasi na kuliandama lango la Kagera huku tukimiliki sehemu kubwa na kutengeneza nafasi lakini wachezaji wetu walikosa umakini.

Endapo nyota wetu Mzamiru Yassin, Shomari Kapombe na Bernard Morrison wangekuwa watulivu katika nafasi tulizopata tungeenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao matatu.

Advertisement

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi tena ambapo dakika ya 45 shuti kali lililopigwa na Morrison lilipaa juu kidogo ya lango la Kagera.

Dakika ya 70 Hamis Kiiza aliwapatia wenyeji bao hilo la ushindi baada ya shambulizi la kushtukiza kufuatia wachezaji wetu kupanda kwenda kushambulia.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Morrison, Mzamiru, Rally Bwalya, Mohamed Hussein na Joash Onyango kuwaingiza Medie Kagere, John Bocco na Yusuf Mhilu, Erasto Nyoni na Hassan Dilunga.

Back to homepage
Share this story