Simba Sports Club
News

Tumepata ushindi mnono dhidi ya Nsingizini

19 Oct 2025

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini mpira ulichezezwa zaidi katikati huku nafasi zikiwa chache zilizotengenezwa.

Wilson Nangu alitupatia bao la kwanza dakika ya 45 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Neo Maema.

Kibu Denis alitupatia bao la pili dakika ya 84 kwa shuti kali akiwa ndani ya sita baada ya kupokea pasi safi ya kisigino iliyopigwa na Jonathan Sowah.

Kibu alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu dakika ya 90 baada ya kupokea pasi ndefu kutoka katikati ya uwanja iliyopigwa na Morice Abraham.

Advertisement

X1: Yakoub, Kapombe, Mligo, Nangu (Chamou 76'), De Reuck, Naby, Mutale (Kibu 65'), Maema (Kagoma 65'), Mwalimu (Sowah 45'), Ahoua (Morice 65'), Mpanzu

Waliionyeshwa kadi:

X1: Tshabalala, Dlamini, Adeleke (Msuvelelo 64') Madondo(Nunadoe 64'), Mavuso, Thwala (Sambulo 79'), Khumalo, Kwakyi, Macina, Shongwe, Gadlela (Quality 69')

Waliionyeshwa kadi: Twala 41' Kwakyi 50' Dlamini 85' Macina 90+6

Back to homepage
Share this story