Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu na matumizi akili na mipango yakiwa makubwa kwa pande zote.
Kutokana na mbinu za makocha wa pande zote timu zilienda mapumziko zikiwa hazijafungana licha ya kosa kosa za hapa na pale.
Kipindi cha pili tulirejea kwa kasi ambapo dakika ya 57 tulipata bao la kwanza lililofungwa na Jonathan Sowah baada ya kupokea pasi kutoka kwa Elie Mpanzu.
Dakika tatu mbele Mpanzu alitupatia bao la pili baada ya kumalizia mpira mrefu uliopigwa na Allasane Kante na kuwazidi ujanja walinzi wa JKT.
Baada ya mabao hayo tuliongeza kasi na kupata mengine ya haraka yalivyofungwa na Ladaki Chasambi, Jean Charles Ahoua, Sowah na Mpanzu tena.
X1: Abel, Duchu, Mligo (Chasambi 60') Chamou, Vedastus (Bashiru 60'), Kagoma (Semfuko 70'), Mutale, Kante (Mzamiru 70'), Sowah (Bajaber 65'), Neo (Ahoua 60') Mpanzu (Awesu 60