Simba Sports Club
News

Tumepata ushindi dhidi ya Fountain Princess

2 Feb 2024

Queens ilipata bao la kwanza dakika ya 12 ambalo kiungo Joelle Bukuru alijifunga katika jitihada za kuokoa mpira uliopigwa Asha Djafar.

Asha Djafar alitupatia bao la pili dakika ya 56 baada ya kupokea pasi kutoka Ritticia Nabbosa ambaye alimfinya beki wa Fountain Gate.

Jentrix Shikangwa alitupatia bao la tatu dakika ya 72 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Nabbosa.

Advertisement

Aisha Mnunka alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Asha Djafar.

Kocha Mussa Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Vaileth Nicholaus, Danai Bhobo, Ritticia Nabbosa Elizabeth Wambui, Fatuma Issa na Jentrix Shikangwa na kuwaingiza Esther Mayala, Ritticia Nabbosa, Mwanahamisi Omary, Joanitah Ainembabazi na Wema Richard.

Back to homepage
Share this story