Simba Sports Club
News

Tumepata ushindi dhidi ya Al Hilal SC

9 Oct 2025

Mchezo ulianza kwa kasi tukishambuliana kwa zamu huku safu zote za ulinzi zikiwa makini kuhakikisha wanakuwa salama

Mshambuliaji Adama Coulibaly aliipatia Al Hilal bao la mapema dakika ya 15 baada ya kupokea mpira nyuma ya walinzi na kufanikiwa kumpiga chenga mlinda mlango, Hussein Abel.

Jean Charles Ahoua alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 31 kwa mpira kona uliotinga wavuni moja kwa moja.

Advertisement

Kipindi cha pili timu zote zilirudi kwa kasi zikitafuta bao la ushindi huku nafasi kadhaa zikitengenezwa ingawa ufanisi haukuwa mzuri.

Jonathan Sowah alitupatia bao la pili dakika ya 85 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Kibu Denis ambaye aliipokea kutoka kwa Bashiri Kibaila.

X1: Abel (Alexander 67'), Kapombe (Duchu 67'), Mligo (Naby 67'), Chamou (Bashiri 67') De Reuck (Vedastus 45'), Kante (Semfuko 67'), Maema (Chasambi 67'), Ahoua (Mbegu 67') Mutale (Mzamiru 67'), Awesu (Mwalimu 35'), Mpanzu (Sowah 67')

Back to homepage
Share this story