Simba Sports Club
News

Tumepata sare dhidi ya ASEC

25 Nov 2023

Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zikishambuliana kwa zamu huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.

Said Ntibazonkiza alitupatia bao letu kwa mkwaju wa penati dakika ya 43 baada ya mpira uliopigwa na Kibu Denis kumgonga mkononi mlinzi wa ASEC.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi ya kutaka kuongeza bao lakini ASEC walikuwa imara nyuma hasa zaidi mlinda mlango wao.

Advertisement

ASEC walisawazisha bao hilo dakika ya 78 kupitia kwa Serge Poku baada ya walinzi wetu kuzembea kuondoa hatari.

X1: Lakred, Israel, Zimbwe Jr, Kennedy, Inonga, Che Malone (Kanoute 57'), Ngoma, Mzamiru (Miqussone 62'), Baleke (Phiri 57'), Ntibazonkiza, Kibu (Chama 71').

Back to homepage
Share this story