Simba Sports Club
News

Tumepata pointi tatu mbele ya KMC

11 Feb 2026

Seleman Mwalimu alitupatia bao la kwanza dakika ya 37 baada ya kumalizia mpira uliookolewa na mlinda mlango Fabian Mutombola baada ya shuti la Libasse Gueye.

Gueye alitupatia bao la pili kwa shuti kali nje ya 18 dakika ya tatu ya nyongeza kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi safi ya kisihino iliyopigwa na Anicet Oura.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga ingawa tulishindwa kuzitumia kuzitumia kikamilifu.

KMC ilimaliza mchezo ikiwa pungufu baada ya mlinzi wa kulia Castor Mwangabo kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 85 kwa kumchezea madhambi Elie Mpanzu.

Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 19 tukiwa nafasi ya sita kwenye msimamo baada ya kucheza mechi nane.

Advertisement

X1: Fabien, Shemvuni, Mudathir, Casto, Mwituka, Chambo, Mwijage (Saliboko 65'), Jammy (Adam 65'), Kidawa, Chibada, Eliuter (Redemtus 65')

Waliionyeshwa kadi: Shemvuni 17' Castor 51' 85'

X1: Abel, Kapombe, Kibabage (Naby 78') Toure, De Reuck, Kagoma (Semfuko 67'), Gueye (Mpanzu 78'), Morice (Loemba 67'), Mwalimu, Chama (Maema 85'), Oura

Waliionyeshwa kadi:

Back to homepage
Share this story