Anicet Oura alitupatia bao la kwanza dakika ya saba baada ya kumalizia mpira uliopigwa kwa kichwa na kiungo Allasane Kante kufuatia Kona iliyopigwa na Clatous Chama.
Mossi Ndumumwe aliisawazishia Singida dakika ya 37 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Lamine Jardju.
Kipindi cha pili timu zote zilirudi kwa kasi zikishambuliana kwa zamu huku tukifika zaidi langoni mwa Singida lakini mlinda mlango Metacha Mnata akiwa kikwazo.
Ushindi huu umetufanya kufikisha alama 27 tukiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza mechi
Elie Mpanzu alitupatia bao la pili dakika 85 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa ndani 18 baada ya kumalizia pasi safi ya Clatous Chama.
X1: Metacha, Koffi, Imoro, Zakaria, Kennedy, Gego, Lamin (Lyanga 86'), Aucho (Rupia 68') Guede, Chukwu, Mossi (Mtange 68')
Waliionyeshwa kadi: Koffi 29' Abdulmalik 45+1' Lamin 83' Chukwu 90+5'
X1: Kassali, Kapombe, Kibabage, Toure, De Reuck, Kagoma, Gueye (Morice 71'), Kante (Mwangosi 53'), Oura, Loemba (Mpanzu 79'), Chama
Waliionyeshwa kadi: Mwangosi 90+5'