Mshambuliaji wa Namungo, Heritier Makambo alishindwa kuendelea na mchezo dakika ya 11 baada ya kupata maumivu nafasi yake ikachukuliwa na Fabrice Ngoy.
Karaboue Chamou alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 43 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Joshua Mutale.
Rushine De Reuck alitupatia bao la pili dakika ya 62 akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Neo Maema.
Mshambuliaji, Seleman Mwalimu alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu dakika ya 83 baada ya kuwazidi ujanja wachezaji wa Namungo na kumpiga chenga mlinzi Hussein Kazi kabla ya kupiga shuti la mguu wa kushoto lililomshinda mlinda mlango, Jonathan Nahimana.
Ushindi huu unatufanya kufikisha alama sita na mabao sita huku tukikaa kileleni mwa msimu.
X1: Yakoub, Kapombe, Mligo, Chamou, De Reuck, Kagoma, Mpanzu (Maema 45'), Kante, Mukwala (Mwalimu 69'), Morice (Ahoua 69'), Mutale (Kibu 69')
Waliionyeshwa kadi: Mligo 82' De Reuck 90+3'
X1: Nahimana, Ondongo (Rogers 71'), Machupa Jr, Kazi, Amoah, Mfuko (Buswita 71'), Masawe, Kiswanya, Makambo (Ngoy 11'), Jofrey, Kabunda (Lukindo 45')
Waliionyeshwa kadi: Mfuko 8' Jofrey 88'