Tulianza mchezo kwa kasi huku huku tukimiliki sehemu kubwa na kutengeneza nafasi za kufunga lakini ufanisi haukuwa mzuri.
Libasse Gueye alitupatia bao la kwanza dakika ya 28 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa nje ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Kibu Denis.
Kibu alipoteza mkwaju wa penati dakika ya 41 iliyochezwa na mlinda mlango Patrick Munthari baada ya Libasse kufanyiwa madhambi na mlinzi Samson Madeleke ndani ya 18.
Seleman Mwalimu alitupatia bao la pili dakika ya 75 akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira uliopigwa na Nickson Kibabage.
Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 16 tukiwa nafasi ya nne baada ya kucheza ya kucheza mechi saba.
X1: Kassali, Duchu, Kibabage, Nangu, De Reuck (Toure 83'), Kagoma, Kibu (Mwalimu 67'), Morice (Chasambi 77'), Oura (Mwangosi 83') , Chama, Libasse (Naby 77')
Waliionyeshwa kadi: Kagoma 87'
X1: Munktari, Gamal, Mpoki, Mohamed, Madeleke, Onditi, Bwenzi (Olomi 60'), Cheda (Ngushi 83'), Kibaya (Mudathir 70'), Balama (Dunia 70'), Kihimbwa
Waliionyeshwa kadi: Onditi 30' Madeleke 52'