Tulianza mchezo huo kwa kasi huku tukitengeza nafasi nyingi na kufika zaidi langoni mwa Prisons katika dakika 15 za mwanzo.
Seleman Mwalimu alitupatia bao la kwanza dakika ya 18 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Inno Jospin Loemba.
Rushine De Reuck alitupatia bao la pili dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati baada ya Shomari Kapombe kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na mlinzi Marco Mhilu.
Kipindi cha pili kasi ya mchezo ilipungua katika dakika 15 za mwisho ingawa tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo.
Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 22 tukiwa nafasi ya nne kwenye msimamo baada ya kucheza mechi tisa.
X1: Mbisa, Sabiyanka (Lukombi 63')Dotto, Jeremia (Mbangula 63'), Mhilu, Mutinda, Sengati, Kimenya, Owino, Mpole (Majanga 81') Chanongo
Waliionyeshwa kadi: Ochu 84'
X1: Kassali Kapombe (Duchu 86') Kibabage, Toure, De Reuck, Kagoma (Semfuko 86') Gueye (Mpanzu 65'), Chama, Mwalimu (Mwangosi 86') Loemba (Maema 72'), Oura
Waliionyeshwa kadi: Kibabage 80'