Mchezo huo ni wa hatua ya awali ya michuano hiyo ambapo kama tukifanikiwa kushinda tutakutana na mshindi kati ya Red Arrows za Zambia na Primero De Agosto ya Angola.
Nyota wetu Peter Banda ametokea timu hiyo mwaka 2021, ambayo imetwaa ubingwa mara 16, akiwa ameichezea kwa mwaka mmoja kabla ya kutolewa kwa mkopo katika timu ya Sheriff Tiraspol kutoka Moldova.
Advertisement
Mchezo wa kwanza utapigwa katika kati ya Septemba 9-11 nchini Malawi na marudiano ni Septemba 16-18.
Tumu ya Big Bullets nao wanatumia jezi nyekundu wakiwa nyumbani na nyeupe ugenini kama sisi.