Tumefanikiwa kutinga hatua hii baada ya kuitoa Greenland kutoka Kagera inayoshiriki Ligi ya Mkoa kwa kuifunga mabao 3-0.
Wapinzani wetu B19 ni timu kutoka jijini Dar es Salaam ambayo inashiriki Ligi Daraja la kwanza (Championship)
Mchezo huo umepangwa kufanyika kati 6-8 Machi ambapo sisi tutakuwa timu mwenyeji.
Advertisement
Mshindi kati ya DodomaJiji na African Sports ndio tutakutana nae katika hatua ya robo fainali endapo tutashinda dhidi ya B19, mchezo ambao utapigwa kati ya 9-14 Aprili.
Malengo yetu kwenye michuano hii ni kuhakikisha tunashinda na kutwaa ubingwa.