Simba Sports Club
News

Tumepangwa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika

28 Dec 2021 By simbasc 9,160 views

Droo ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika imekamilika mchana huu jijini Cairo Misri na tumepangwa kundi D.

Kikosi chetu kimepangwa kundi D pamoja na timu za RS Berkane ya Morocco, Asec Mimosas ya Ivory Coast pamoja na USGN ya Niger.

Advertisement

Mchezo wetu wa kwanza utafanyika jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Februari 13 mwaka 2022, dhidi ya Asec Mimosas.

Timu mbili za juu katika kundi letu zitaingia moja kwa moja hatua ya robo fainali.

Back to homepage
Share this story