Simba Sports Club
News

Tumepangwa Kundi C Mapinduzi Cup

15 Dec 2022

Kila mwaka michuano hiyo huanzia mwanzoni mwa mwaka na kukamilika siku moja baada ya sherehe za Mapinduzi ambazo hufanyika Januari 12.

Msimu huu michuano ya Mapinduzi itashirikisha timu 12 huku tano zikitoka Tanzania Bara, Sita kutoka Visiwani na moja kutoka nchini Burundi.

Advertisement

Sisi ndio mabingwa watetezi na tumepangwa pamoja na timu za Mlandege pamoja na KVZ zote kutoka Visiwani Zanzibar.

Mchezo wetu wa kwanza utakuwa Januari 3 dhidi ya Mlandege na Januari 5 tutamaliza na KVZ.

Back to homepage
Share this story